Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame DPRK waathiri uzalishaji wa chakula:FAO

Ukame DPRK waathiri uzalishaji wa chakula:FAO

Uzalishaji wa chakula nchini Jamhuri ya watu wa Korea au DPRK umeathirika pakubwa na ukame mbaya kuwahi kuikumba nchini hiyo tangu mwaka 2001, limesema leo shirika la chakula na kilimo (FAO).

Mvua katika maeneo muhimu ya uzalishaji wa chakula DPRK iliyonyesha chini ya kiwango kuanzia mwezi April hadi Juni mwaka huu imevuruga msimu wa upanzi na kuharibu mazao yakiwemo ya chakula kikuu kama mpunga, mahindi, viazi na maharage.

Kwa mujibu wa FAO na mshirika wake tume ya Muungano wa Ulaya, endapo mvua hizo hazitoimarika mapema, uzalishaji wa nafaka huenda ukapungua kwa kiasi kikubwa sana na kuhatarisha zaidi hali ya uhakika wa chakula nchini humo.