Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola milioni 11 zatolewa na Marekani kupambana na njaa CAR

Dola milioni 11 zatolewa na Marekani kupambana na njaa CAR

Serikali ya Marekani imetoa dola milioni 11 zitakazowasaidia watu zaidi ya laki tano nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kupambana na tatizo la njaa linaloongezeka wakati machafuko mapya yakizuka.

Likikaribisha mchango huo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesema fedha hizo zilizotolewa na USAID, zaitaisaidia WFP kusaidia watu laki tano unusu katika nchi nzima ya CAR wakiwemo wakimbizi wa ndani , wakimbizi wa kawaida, wanafunzi na jamii zinazohifadhi wakimbizi zisizojiweza kabisa.

Shirika hilo limeongeza kuwa fedha hizo sio tu zitasaidia mgao wa chakula bali pia kutoa mlo mashuleni na juhudi za kurejea katika maisha ya kawaida kwa jamii ambako sasa vita vimepungua, ikiwemo miradi itakayowasaidia wakulima wadogowadogo kurejea tena katika kilimo.

Mwaka huu wa 2017 WFP inalenga kuwafikia watu 700,000 nchini CAR kwa msaada wa chakula na lishe.