Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

SDG’s ni muhimu sana kwa FAO na mustakhbali wa dunia:Semedo

SDG’s ni muhimu sana kwa FAO na mustakhbali wa dunia:Semedo

Malengo yote ya maendeleo endelevu ni muhimu sana kwa shirika la chakula na kilimo FAO, lakini yanayopewa kipaumbele zaidi ni leongo nambari 1 kutokomeza umasikini, 2, kumaliza njaa, 13 la mabadiliko ya tabia nchi , 14 masuala ya viumbe baharini na namba 15 linalohusu maisha nchi kavu hasa bayoanuai.

Hayo yamesemwa na Maria Helena Semedo naibu mkurugenzi mkuu wa FAO anayehudhuria mkutano wa ngazi ya juu wa kisiasa kuhusu tathimini ya utekelezaji wa SDG’s unaoendelea hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Bi Semedo amesema ukizingatia utekelezaji wa malengo haya umeanza miaka miwili iliyopita hatua zimepigwa lakini

(CUT YA MARIA SEMEDO)

“Tunahitaji kubadilika jinsi tunavyofanya kazi, tunavyofanya biashara kuwa na mtazamo wa muingiliano wa sekta mbalimbali, siku zote sio rahisi lakini lazima tuachane na kujitenga, katika ngazi ta kitaifa lakini pia kimataifa , naweza kutaja kwenye Umoja wa Mataifa ambako tunatakiwa kufanya kazi kama kitu kimoja, kwa sababu malengo yote ya SDG’s yanahusiana.”