Jukwaa la kupinga ugaidi mitandaoni limekuja wakati muafaka-UM

27 Juni 2017

Umoja wa Mataifa umekaribisha jukwaa la kimataifa la mtandao wa intanet katika kukabiliana na ugaidi, juhudi ambazo zinawalenga watumiaji wa mitandao hiyo kutounga mkono  magaidi na wenye misimamo mikali kwa watumiaji wa mitandao mbalimbali.

Kampuni inayounda jukwaa hilo ni Facebook, Twitter na YouTube na Microsoft.

Akikaribisha hatua hiyo Mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa cha kukabiliana na ugaidi Jean-Paul Laborde, amesema jukwaa hilo ni muendelezo wa ubia uliopo kati ya  umoja huo na sekta za umma na binafsi katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Amesema ugaidi ni tishio la dunia ambalo laweza kutokomezwa kwa juhudi endelevu pekee, na kuwakaribisha wadau wengine wa sekta binafsi kuungana katika kufanikisha lengo hilo.

Mkuu huyo wa makabiliano dhidi ya ugaidi katika Umoja wa Mataifa amesema baraza la usalama la umoja huo linaunga mkono hatua hiyo hasa kwa kuzingatia kuwa baraza hilo lilipitisha hivi karibuni azimio namba 2353 linalotoa mkakati wa kukabiliana na masuala ya ugaidi na vitendo vyote vinavyotishia amani na usalama wa dunia.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter