Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi Tisa zikiwemo Tanzania na DRC kuchangia ongezeko la idadi ya watu duniani- Ripoti

Nchi Tisa zikiwemo Tanzania na DRC kuchangia ongezeko la idadi ya watu duniani- Ripoti

Katika miaka sita ijayo, India itaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu duniani na hivyo kuipiku China. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa hii leo kama anavyoelezea Amina Hasssan.

(Taarifa ya Amina)

Kubwa katika ripoti hiyo inayoangazia makadirio ya idadi ya watu ni kwamba wakazi wa dunia wataongezeka kutoka bilioni 7.6 hivi sasa hadi bilioni 8.6 mwaka 2030, kipindi ambacho ni ukomo wa malengo ya maendeleo endelevu.

Hata hivyo ifikapo mwaka 2024 India inatarajiwa kuipiku China na kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu duniani.

Na zaidi ya yote nchi zinazochangia ongezeko hilo la idadi ya watu duniani ni Tisa tu zikiongozwa na India, Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Pakistan, Ethiopia, Tanzania, Marekani, Uganda na Indonesia.

Ripoti hiyo imebainisha hata hivyo kupungua kwa kiwango cha uzazi kwenye maeneo yote hata barani Afrika kutoka wastani wa watoto 5.1 kwa mwanamke mmoja mwaka 2000 na 2005 hadi watoto 4.7 mwaka 2010 na 2015.