Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima Nigeria wapatiwa pembejeo za kilimo

Wakulima Nigeria wapatiwa pembejeo za kilimo

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesambaza mbegu za mazao na mbolea kwa zaidi ya wakulima zaidi ya milioni moja huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria ambako mashambulio ya Boko Haram yamesababisha uhaba wa chakula.

Mwakilishi mkazi wa FAO nchini Nigeria Nourou Macki Tall amesema msaada huo wa pembejeo umewezekana baada ya Ujerumani kutoa dola milioni 4.5 kukwamua hali ya ukosefu wa chakula kwenye majimbo ya Adamawa, Borno na Yobe kwenye eneo hilo.

FAO imesema msaada huo utawezesha wakulima kupanda mazao yao wakati wa msimu huu wa upanzi na hivyo kuondokana na njaa na utapiamlo siku za usoni.

Takribani watu milioni 5.2 kwenye majimbo hayo wanakabiliwa na ukosefu wa chakula na hivyo wanahitaji msaada wa haraka.