Ulinzi wa amani unasalia chapa ya Umoja wa Mataifa-Guterres

24 Mei 2017

Katika kuadhimisha Siku ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa, ambayo kila mwaka hua Mei 29, leo Umoja huo unawaenzi walinda amani 117 kutoka nchi 43 waliofariki mwaka jana pekee wakati wakitekeleza jukumu la amani sehemu mbalimbali duniani. Assumpta Massoi na taarifa kamili

(TAARIFA YA ASSUMPTA)

Nats!

Ukimya na hisia vimetawala katika ukumbi huu, walinda amani wakiwa wamevalia maazi ya kijeshi wakiwaenzi mashujaa wenzao waliotangulia mbele ya haki kishujaa.

Hadhira hii ilikaa kimya kwa dakika moja kwa heshima ya walinda amani hao.

Kisha nchi zilizopoteza walinda amani zikakabidhiwa medali kwa kutajwa majina

Nats!

Awali Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António amesema kofia ngumu ya bluu inayovaliwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa inasalia kuwa chapa muhimu ya umoja huo na kazi ya thamani inayofanywa na kundi hilo itaenziwa daima akisema

( Sauti Guterres)

‘‘Lazima tuendelee kuwekezeka katika usalama wa walinda amani wetu, familia za walinda amani, operesheni za amani na msaada mashinani . Makao makuu ya Umoja wa Mataifa na nchi wanachama lazima wafanye kazi pamoja kufanya ulinzi wa amani salama kadri iwezekanavyo.’’

Hafla hii inafanyika siku moja baada ya shambulio dhidiya walinda amani wa ujumbe wa Umohja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA, ambapo walinda amani wawili kutoka Chad wameuwawa.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter