Chuja:

Siku ya Walinda Amani

Private  Monica Constantino Nyagawa, analinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC chini ya bendera ya Umoja wa MAtaifa. Yeye anatoka Tanzania.
MONUSCO

Amani ni pamoja kuwapatia huduma za afya wananchi DRC- Mlinda amani TANZBATT_8  

Walinda amani wa Tanzania wanaohudumu katika kikosi cha 8, TANZBATT_8 kwenye Brigedi ya kujibu mashambulizi, FIB ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO wamezungumzia kile ambacho wanafanya katika kusongesha jukumu la Umoja wa Mataifa la kulinda amani kwenye taifa hilo lililogubikwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwa miongo kadhaa sasa.

UN/UNIC Nairobi

Nilipokea taarifa za ushindi nikwa nyumbani na kwa kweli nilijawa nafuraha sana-Meja Nyaboga

Chanda chema huvikwa pete walinena wahenga na hali ni kama hiyo kwa mlinda amani kutoka Kenya ambaye amechaguliwa kupokea tuzo ya Umoja wa Mataifa ya mwanajeshi mwanaharakati wa masuala ya kijinsia kwa mwaka 2020.  

Meja Steplyne Nyaboga ambaye alikuwa mshauri wa kijeshi wa masuala ya kijinsia alipohudumu katika operesheni ya Umoja wa Mataifa ya mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wa kulinda amani Darfur (UNAMID) katika mahojiano maalum na Grace Kaneiya akiwa huko Nairobi Kenya amesema alipokea habari za ushindi, “kwa furaha isiyo kifani” 

Sauti
3'43"
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiweka shada la maua kwenye hafla ya kuwaenzi na kuadhimisha siku ya walindamani duniani
UN Photo/Mark Garten)

UN yaenzi kujitolea na ujasiri wa walinda amani

Mchango wa vijana katika kuleta amani haupingiki na kuanzia Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC mpaka Lebanon, walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanafanya kazi na vijana kupunguza machafuko na kudumisha amani, ikiwemo upokonyaji wa silaha, kuwakusanya na kuwarejesha tena katika jamii na kuwaingiza katika program za kupunguza machafuko katika jamii.

MINUSMA/Harandane Dicko

Asanteni Vijana kwa kulinda amani: Guterres

Katika kuelekea siku ya walinda amani dunaini Tarehe 29 mwezi huu wa Mei, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema mchango wa vijana katika kudumisha amani ni mkubwa na amani haiwezi kupatikana endapo hawatoshirikishwa. Tupate ufafanuzi zaidi kutoka kwa Flora Nducha. 

Baadhi ya vijana Sudan Kusini wakipaza sauti zao na kusisitiza umuhimu ushirikishwa katika jamii wakisema wana mchango mkubwa katika kila nyanja ya maisha ikiwemo masuala ya ulinzi wa amani. 

29 Mei 2020

Kwenye Jarida la Umoja wa Mataifa leo ni siku ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa duniani :

-kwenye mada yetu ya kina baadhi ya wanawake wakazi wa mji wa Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wameomba walinda amani wanawake kutoka Tanzania waendelee kuwaunga mkono kiuchumi na kijamii.

-Mlinda amani mwanamke kutoka Tanzania ambaye anahudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO amethibitisha umuhimu wa uwepo wa askari wa kike katika ulinzi wa amani

Sauti
9'56"