Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya watu waliofurushwa makwao Mosul imezidi uwezo wa kuwasaidia – UM

Idadi ya watu waliofurushwa makwao Mosul imezidi uwezo wa kuwasaidia – UM

Idadi ya watu waliolazimika kuhama makwao kutokana na mapigano katika mji wa Mosul nchini Iraq imezidi uwezo wa usaidizi wa kibinadamu, amesema mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini humo, Lise Grande.

Kwa mujibu wa Bi Grande, takriban watu 700,000 wamekimbia makwao tangu operesheni za kijeshi zilipoanza mwezi Oktoba mwaka 2016, zikilenga kuunyakua tena mji wa Mosul kutoka wapiganaji wa ISIL.

Idadi hiyo inajumuisha watu nusu milioni kutoka magharibi mwa mji pekee.

Wengi wa waliofurushwa makwao wanahitaji chakula, na hawajaweza kupata maji safi ya kunywa na dawa kwa kipindi cha wiki kadhaa au hata miezi.

Kufikia sasa, ombi la dola milioni 985 kwa ajili ya huduma za kibinadamu Iraq limefadhiliwa kwa asilimia 30 tu.