Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Barubaru 3000 hufariki dunia kila mwaka kwa sababau zinazozuilika-WHO

Barubaru 3000 hufariki dunia kila mwaka kwa sababau zinazozuilika-WHO

Ripoti mpya ya shirika la afya ulimwenguni WHO na wadau wake inasema kwamba zaidi ya vijana barubaru 3000 hufa kila siku , ikiwa ni sawa na vifo milioni 1.2 kwa mwaka, kutokana na sababau zinazoweza kuzuilika, huku idadi kubwa ya vifo ikiwa katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati. Amina Hassan na taarifa zaidi

( TAARIFA YA AMINA)

Ripoti hiyo iliyotolewa leo inasema mwaka 2015 zaidi ya theluthi mbili ya vifo viliripotiwa barani Afrika ma Kusini Mashariki mwa bara Asia, huku ajali za barabarani, maambukizi ya mfumo wa kupumua, na kujiua vikitajwa kuwa sababu kuu za vifo vya barubaru hao.

Imependekeza kwamba vifo vingi vyaweza kuzuilika kwa kuwa na huduma bora za afya, elimu na usaidizi wa kijamii lakini katika maeneo mengi kundi hilo ambalo hukabiliwa na magonjwa ya afya ya akili, matumizi ya dawa za kulevya, au lishe duni hawapati kinga na huduma mujarabu kwasababu ya ukosefu wa huduma au ukosefu wa elimu kuhusu huduma hizo.

Dk Anthony Costello ni Mkurugenzi Msaidizi wa WHO kuhusu uzazi, watoto na barubaru.

( Sauti Dk Anthony)

‘‘Ripoti yetu inaenda mbali zaidi ya vifo, kinachokosekana hapa ni fursa kubwa katika kukabiliana sio tu na matatizo yaafaya kwa barubarau lakini pia vyanzo vya magonjwa mengi ambayo tunakabiliana nayo katika utu uzima. Ukifikiri kuhusu magonjwa ya moyo, kiharusi, kisukari na saratani. Tabia nyingi ambazo huanza katika umri wa barubaru zaweza kudhibitiwa na kuokoa uchumi.''