Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sitisho la mapigano litumiwe kusaka amani Syria: de Mistura

Sitisho la mapigano litumiwe kusaka amani Syria: de Mistura

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria Staffan de Mistura amesema mpango mpya wa kusitisha mapigano nchini Syria waweza kusaidia katika mazungumzo mengine mjini Geneva,Uswisi.

Amesema ikiwa fursa hiyo haitatumiwa kwa manufaa, vita hiyo yaweza kushuhudia kuibuka kwa maeneo mengine 10 yanayofanana na kinachoendelea Aleppona hivyo kuzidisha madhila kwa wananchi kutokana na machafuko kati ya vikosi vya serikali na vile vya upinzani ambapo matakwa ya udhibiti mji wa Aleppo yamesababisha kero zaidi mwaka jana.

Kiongozi huyo amewaambia wanahabari mjini Geneva kwamba kuna jambo la upekee katika makubaliano ya sitisho la mapigano lililotiwa saini na Urusi, Uturuki na Iran mjini Astana kwani ni nchi zenye ushawishi kuhusu Syria.

Hata hivyo de Mistura ameonya kuwa maachafuko zaidi yaweza kuwepo akisema.

( Sauti de Mistura)

‘‘Waharibifu watakuwepo, waharibifu wapo, lakini hilo lisiwe chachu ya kutotoa angalau tumaini. Kuna mbinu mbadala katika hilo, ambayo ni kurejea kwenye Allepo 10, Mungu aepushie mbali Allepo.’’

Awamu ya pili ya majadiliano ya kusaka suluhu ya Syria yatafanyika mnmoa Mei 16 mjini Geneva nchini Uswisi.