Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wadau wa kimataifa kujadili mustakhbali wa Somalia mjini London

Wadau wa kimataifa kujadili mustakhbali wa Somalia mjini London

Wadau wa kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika, serikali ya Uingereza , Somalia na wengine wanaounga mkono mustakhbali wa Somalia wanakutana London wiki hii kujadili hatma ya taifa hilo la Pembe ya Afrika lililoghubikwa na vita vya zaidi ya miongo miwili .

Mkutano huo wa kimataifa ambao utaanza rasmi Mei 11utaongozwa na Muungano wa Afrika, serikali ya Somalia, Uingereza mwejeji na mwenyiki mwenza atakuwa Umoja wa Mataifa. Utajikita katika mada mbalimbali kama anavyofafanua mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Michael Keating

(SAUTI YA KEATING )

“lengo ni kutoa fursa kwa serikali mpya ya Somalia kuweka vipaumbele vyake , pia kujadili ushirika baina ya Somalia na jumuiya ya kimataifa katika maeneo mbalimbali ikiwemo sio tu kukabiliana na ukame bali pia kuwekeza katika uchumi, suala la usalama na katika masuala muhimu ya kisaisa , lakini pia kujaribu kuleta amani na maridhiano Somali"

Je kwa Wasomali wenyewe nini matarajio yao katika mkutano huo? Sagal Bihi ni mbunge wa shirikisho la serikali ya Somalia

(SAUTI YA SAGAL)

"Asilimia kubwa ya jamii ya Wasomali ni vijana na wanaathirika moja kwa moja na kutokuwepo kwa usalama na maendeleo ya kiuchumi, kitu kikubwa tunachotarajia kwenye mkutano wa London ni kuhakikisha Somalia inakuwa na amani na usalama wa muda mrefu ili tuweze kufufua tena uchumi, endapo tutawawezesha vijana kuwapa elimu na fursa za ajira nitafurahi sana endapo tutaona matokeo baada ya mkutano wa London"