Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi ya 200 hawajulikani waliko baada ya meli zingine mbili kuzama:UNHCR

Watu zaidi ya 200 hawajulikani waliko baada ya meli zingine mbili kuzama:UNHCR

Katika saa 24 zilizopita shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limepokea taarifa za kusikitisha kuhusu mabaki ya meli zingine mbili Katikati mwa bahari ya Mediterranean. Joseph Msami na taarifa kamili

(TAARIFA YA MSAMI)

Kwa mujibu wa UNHCR ajali ya kwanza ilitokea Ijumaa usiku wakati boti iliyosafiri kwa saa kadhaa ikiwa na watu 132 kuzama. Watu 50 waliokolewa na kupelekwa Pozzallo (Sicily) italia Jumapili lakini watu wengine 82 wanahofiwa kufa maji au kutojulikana walipo.

Ajali ya pili imetokea kwenye mwambao wa Libya Jumapili , ambapo mwanamke mmoja na wanaume sita waliokolewa huku watu wengine 163 wakihofiwa kufa au kupotea baharini. Cécile Pouilly ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI CECILE POUILLY)

“Kama tulivyosema mara nyingi siku za nyuma operesheni za ukozi baharini ni muhimu sana zinaokoma maisha ya maelfu ya watu na tunapongeza juhudi za askari wana maji wa Italia pamoja na kazi kubwa inayofanya na NGO’s”.

Nalo shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema mwaka huu hadi kufikia Mei 7 watu 49, 3010 wameingia Ulaya kupitia Mediterranean wengi wakiwasili Italia, Ugiriki, Cyprus na Hispania na zaidi ya 1300 kupoteza maisha.