Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dhana potofu dhidi ya wahamiaji kikwazo cha mkakati wa kuwalinda:UM

Dhana potofu dhidi ya wahamiaji kikwazo cha mkakati wa kuwalinda:UM

Umoja wa Mataifa umesema leo Jumatatu kwamba ukosefu wa ulinzi dhidi ya wahamiaji duniani na kushindwa kuikabili dhana potofu dhidi ya kundi hilo vinahitaji kushughulikiwa kwa manufaa ya kila mmoja.

Akizungumza na nchi wanachama mjini Geneva Uswisi, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kupigia chepuo haki za binadamu za wahamiaji wote,Louise Arbour ambaye ni mwanaharakati wa umoja huo kuhusu uhamiaji wa kimataifa, amesema kuna sheria nyingi za kimataifa za kuwezesha kuwanzishwa kwa mkakati wa dunia wa wahamiaji ambao uliahidiwa na jumuiya ya kimataifa kutekelezwa mwaka ujao

Sheria hizo ni tamko la kimataifa la haki za binadamu, na sheria za kimataifa zinazoongoza wafanyakazi, uhalifu na mambo ya bahari.

Bwana Arbour ameongeza kwamba licha ya uwepo wa sheria hizo na utashi wa kisiasa wa kushughulikia uhamiaji, bado kuna pengo la utekelezaji wa ulinzi wa haki za binadamu katika kundi hilo.

Amesema kuna ukosefu wa haki za dhahiri kwa wahamiaji hutokana na dhana potofu na kuongeza kuwa hiyo husababaisha wakose huduma za afya, nyumba, elimu na haki.

Mkutano huo wa zaidi ya siku mbili ambao huzileta pamoja nchi na wadau wengine wa masuala ya wahamiaji kama vile asasi za kiraia, unafuatia tamkao L New York kuhusu wakimbizi na wahamiaji ambalo lina lengo la kuanzishwa kwa mkakati wa kimataifa wa usalama na sheria za wahamiaji mnamo mwaka 2018.