Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maisha ya binadamu yanategemea uhai wa dunia-UM

Maisha ya binadamu yanategemea uhai wa dunia-UM

Binadamu ni wabinafsi sana linapokuja suala la uhusiano wao na mali asili , kwa sababu ya kushindwa kwao kuelewa kwamba wao ni sehemu  asili ya dunia, amesema Wu Hongbo, msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika idara ya uchumi na masuala jamii.

Hongbo ametoa kauli hiyo wakati wa mjadala wa baraza kuu wa “amani na asili” katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya Mama Dunia ambayo kila mwaka ni Aprili 22.

Mada ya mjadala huo ni “filosofia ya kisheria ya dunia” ni suala linaloibuka kisheria ambalo linaiona na kuichukulia dunia kama chombo cha msingi chenye haki na sio kitu cha kutumiwa vibaya.

Maadhimisho kote duniani ya siku ya kimataifa ya Mama Dunia ni kumbusho la jukumu muhimu linalobebwa na dunia kwa kutoa uhai endelevu kwa wote umesema Umoja wa Mataifa. Siku hii pia inachagiza kuwa na amani na mazingira na dunia. Hongbo amesisitiza

(SAUTI HONGBO)

"Sisi ni sehemu ya maisha aya asili ya dunia. Kushindwa kwetu kuelewa ina maanisha nini kuwa sehemu ya dunia ya asili kumetufanya kuwa na mahusiano na mali asili kwa maslahi nbinafsi mawazoni mwetu. Naridhika kuona kwamba zaidi na zaidi nchi zimechukua hatua kuweka sawa hali hii ikiwemo kutoa haki ya kisheria kwa mali asili.”

Ecuador ilikuwa nchi ya kwamnza kutambua haki za mali asili katika katiba ya nchi yake na Bolivia imepitisha sheia nyingi kuhusu haki za mali asili.