Kupitishwa kwa Baraza la mawaziri Somalia ni hatua chanya- UM

31 Machi 2017

Umoja wa Mataifa umekaribisha hatua ya Bunge la Somalia kupitisha Baraza la Mawaziri lililoteuliwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hassan Ali Khaire mapema mwezi huu.

Baraza hilo lina mawaziri 27 ambao sita kati yao ni wanawake, hatua ambayo Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa umoja huo nchini Somalia, Michael Keating amesema ni chanya katika kuwezesha kisiasa wanawake wa nchi hiyo ya pembe ya Afrika.

Idadi hiyo ya wanawake kwenye Baraza la Mawaziri ni kubwa kuwahi kujumuishwa kwenye serikali ya shirikisho Somalia.

Halikadhalika Bwana Keating amesema kwa kuridhiwa baraza hilo, ina maana sasa serikali itatekeleza mpango wa serikali uliowasilishwa kabla ya kupitishwa kwa baraza ambao unajumuisha kutokomeza umaskini na kuchagiza mapitio ya katiba ili upigaji kura wa kila mwananchi ufanyike mwaka 2020.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud