Skip to main content

Shilingi 5,000 zimebadili maisha yangu: Mjasiriamali

Shilingi 5,000 zimebadili maisha yangu: Mjasiriamali

Mjasiriamali kutoka Tanzania Bi Amina Shaaban anasema amefanikiwa kusomesha watoto wake kwa kuanzia na mtaji wa shilingi 5,000 za Tanzania ambapo aliitumia kuuza nazi nakupata faida.

Bi Amina ni miongoni mwa wanawake wa Tanzania Zanzibar, hususani Pemba, ambao wamenufaika baada ya serikali kuelimisha wanawake namna ya kujikomboa kiuchumi ili kukabiliana na chnagamoto ya ajira.

Ungana na Khadija Kombo wa redio washirika Micheweni redio ya Pemba katika makala itakayokupa undani wa taarifa hii ya kusisimua.