Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Radio ya UM ni chombo muhimu kwa dunia:Wasikilizaji DRC

Radio ya UM ni chombo muhimu kwa dunia:Wasikilizaji DRC

Tangu mapema miaka ya 1950 ilipoanzishwa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa imekuwa msitari wa mbele sio tuu kujulisha ulimwengu shughuli za Umoja wa Mataifa na mashirika yake bali pia kuelimisha, kuhabarisha, kuburudisha, kutoa msaada na hata kuwapa fursa wasikilizaji kutoa maoni na madukuduku yao kuhusu Umoja wa Mataifa.

Leo hii Idhaa ya Kiswahili inabisha hodi mjini Bukavu jimbo la Kivu Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambako baadhi ya wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili wameamua kuunda club maalumu ya wasikilizaji.

Ili kufahamu ni kwa nini wakaamua kuunda club hiyo na wanavyofaidika na Radio ya Umoja wa Mataifa Flora Nducha amezungumza na baadhi yao , wasikilize.