Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Stadi za kazi kambini zamwezesha mkimbizi mwanamke kujikimu

Stadi za kazi kambini zamwezesha mkimbizi mwanamke kujikimu

Kuelekea siku ya wanawake duniani tarehe 08 mwezi huu wa machi, mwanamke mmoja mkimbizi kutoka Burundi ameelezea vile ambavyo stadi za kazi kambini zimemwezesha kuungana tena na familia yake.

Mahimana Faines ambaye sasa anaishi kambi ya wakimbizi ya Lusenda nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC amesema anasema kupitia kituo salama kambini Lusenda alipata taarifa za uwepo wa ajira ndogo ndogo pamoja na stadi za ujasiriamali ambazo zilimpatia uwezo wa kutengeneza bidhaa kama sabuni ambazo zilimpatia kipato.

( Sauti Faines)

Amesema alifahamu kuwa kwa kufanya kazi angeweza kupata pia fedha ya kurejea Burundi ili kuweza kuwachukua watoto wake wengine wanne alioshindwa kuondoka nao wakati akikimbia mapigano.

Bi. Mahimana amesema tayari ameweza kuwachukua watoto wake na kwamba matumaini yake katika kambi hiyo ni jinsi ambavyo kituo salama kinawapatia fursa wanawake kufarijiana na kuweza kumudu maisha ya ukimbizini.

( Sauti Faines)