Wanawake waongezeka katika mabunge, kasi zaidi yahitajika: IPU
Hatua zaidi na utashi thabiti wa kisiasa unahitajika, kuwezesha uwakilishi wa wanawake bungeni ili kuendeleza kasi ya maendeleo yaliyofikiwa duniani katikaa kipindi cha muongo mmoja uliopita, umesema muungano wa mabunge duniani IPU.
Katika ripoti ya IPU kuhusu tathimini ya mwaka huu iitwayo Wanawake bungeni 2016, iliyotolewa kuelekea siku ya wanawake duniani Machi nane hapo kesho, taasisi hiyo imetaka uhuishwaji wa kasi kuhakikisha sauti za wanawake zinajumuishwe katika michakato ya umuzi.
Kwa mujibu wa IPU, wastani wa wanawake katika mabunge duniani uliongezeka kutoka asilimia 22.6 mwaka 2015 hadi 23.3 mwaka jana, ambapo pia miaka 10 iliyopita idadi ya wanawake ilikuwa asilimia 16.8 duniani hii ikimaanisha asilimia 6.5 imeongezeka katika muongo mmoja.
Ripoti hiyo hata hivyo imesema katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mafanikio hafifu, na hiyo kutaka juhudi zaidi ili kufanikisha usawa wa kijinsia katika siasa.