Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madhila kwa wajawazito Lubumbashi DRC ni mengi:Dr Tshanda

Madhila kwa wajawazito Lubumbashi DRC ni mengi:Dr Tshanda

Waswahili husema asifiaye mvua imenyea, au siri ya mtungi aijuaye kata. Kwa kila mama wajawazito mjini Lubumbashi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, adha ya kukosa huduma muhimu kwa kutokuwa na fedha imekuwa kawaida, maisha yao na watoto wao yakiwa hatarini kila uchao.

Lakini sasa wameanza kupata matumaini baada ya Dr Micrette Ngalula-tshanda ambaye pia ni mama wa watoto watano kuamua kuanzisha kliniki kwa ajili ya wajawazito na watoto inayotoa huduma bure bila ghara yoyote. Dr tshanda yuko hapa New York kuhudhuria kikao cha 61 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW61 amezungumza na Flora Nducha wa idhaa ya Kiswahili kuhusu shughuli ya kujitolea anayoifanya

(MAHOJIANO NA DR MICRETTE)