Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wanaotawanywa na machafuko kwa siku Mosul ni 4,000

Watu wanaotawanywa na machafuko kwa siku Mosul ni 4,000

Idadi ya watu wanaotawanywa kwa siku Mosoul Iraq kutokana na operesheni za kijeshi zinazoendelea dhidi ya kundi la kigaidi la ISIL na hofu ya matumizi ya silaha za ckemikali dhidi ya raia imeongezeka sana.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR sasa watu 4000 kwa siku wanakimbia kutoka Magharibi mwa Mosoul sehemu ambayo kwa kiasi kikubwa inadhibitiwa na waasi wenye itikati kali.

Idadi ya watu hao wanaotawanywa inakadiriwa kuwa zaidi ya 191,000, huku takribani 100,000 kati ya hao ni watoto limesema shirika l Umoja wa mataifa a kuhudumia watoto UNICEF.

Wakati huohuo kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekuendu ICRC imelaani vikali matumizi ya silaha za kemikali katika mgogoro wa Mosoul. Iimesema wagonjwa watano wanaopatiwa matibabu karibu na hospital ya Mosoul wakiwemo watoto watatu na wanawake wawili dalili zao ni vidonda, macho mekundu, muwasho , kutapika na kukohoa.