Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sheria kali zahitajika kulinda wanyamapori- UM

Sheria kali zahitajika kulinda wanyamapori- UM

Leo ni siku ya wanyamapori duniani, inayotumiwa kukuza uelewa kuhusu wanyama pori na mali asili kwa lengo la kuhifadhi viumbe hao. Kauli mbiu ya mwaka huu ni kusikiliza sauti za vijana. Rosemary Musumba na maelezo zaidi.

(TAARIFA YA ROSE)

Hawa ni ndovu, moja ya wanyama vivutio duniani, lakini wanyama hawa wanakabiliwa na tishio la kutoweka ikiwa hatua za kuwalinda hazitachukuliwa, ndiyo maana Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonjo Guterres katika ujumbe wake kuhusu siku ya wanyama pori duniani anasema ujangili na usafirishaji haramu wa wanayamapori hasa wale ambao ni alama na vivutio vya dunia ni tishio na hivyo sheria kali zahitajika.

Na hawa ni vijana, wakipaza sauti ya ulinzi dhidi ya wanayamapori na maliasili.

Nchini Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP kwa kushirikiana na wizara ya maliasili na utalii na wadau wengine, wameadhimisha tukio hilo kwa mkutano uliojadili juhudi za kukabiliana na ujangili.

Clara Makenya ni Afisa mwakilishi wa UNEP Tanzania .

( Sauti Clara)

Kwa upande wake waziri wa maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe amezungumzia umhimu wa ubia na sekta binafsi katika kuhifadhi wanyamapori na maliasili.

(Sauti Profesa Maghembe)