Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wavukao Mediteranea wakumbwa na ukatili wa kupindukia- UNICEF

Watoto wavukao Mediteranea wakumbwa na ukatili wa kupindukia- UNICEF

Safari ya watoto wanaokimbia mizozo na mateso Afrika kwenda Ulaya kupitia bahari ya Mediteranea imegubikwana mateso ikiwemo ukatili wa kingono na utumikishwaji, imesema ripoti mpya ya shirika la kuhudumia watoto duniani, UNICEF iliyotolewa hii leo.

Ikipatiwa jina safari ya hatari ya watoto kupitia njia ya wahamiaji ya Mediteranea, ripoti hiyo inaeleza kwa kina hatari wanazokumbana nazo watoto wakimbizi wanaposafiri kupitia jangwa la Sahara, Libya na hatimaye kuvuka bahari kuingia Italia.

Mmoja wa watoto anasimulia…

(Nats)

image
Mmoja wa watoto aliyesimulia masahibu yanayowakumba njiani. (Picha:Unicef video capture)
Anasema alifahamu kuwa ni hatari kwenda Italia kwa boti lakini aliamini kuwa akifika Ulaya ataanza maisha bora..

Robo tatu ya watoto waliohojiwa wamesema hukumbwa na manyanyaso na ukatili miongoni mwa watu wazima. Afshan Khan, mkurugenzi wa UNICEF akihusika na janga la wahamiaji Ulaya mwishoni mwa wiki alijionea hali halisi ya watoto hao Italia na anataja moja ya mapendekezo yao..

(Sauti ya Afshnan)

“Tunaushawishi Muungano wa Ulaya utenge rasilimali kuimarisha mipango ya ulinzi wa mtoto nchini Libya ili kuzuia watoto walio hatarini zaidi na pia kuinua uwezo kwenye vituo vya mapokezi na malezi.”

Mapendekezo mengine matano ni ulinzi wa watoto wakimbizi na wahamiaji wanaosafiri peke yao, kuondokana na ushikiliaji watoto wanaosaka hifadhi, kuweka familia pamoja kama njia ya kulinda watoto, kuchukua hatua dhidi ya vichochezi vya ukimbizi na uhamiaji.