Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba wa kimataifa kurahisisha biashara waanza kutumika-UNCTAD

Mkataba wa kimataifa kurahisisha biashara waanza kutumika-UNCTAD

Wajumbe wa shirika la biashara duniani WTO, wakiungwa mkono na kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD, wamejitoa kimasomaso kurahisisha taratibu ambazo kwa kiasi kikubwa zitangeza biashara ya kimataifa, kupunguza rushwa na kuongeza maendeleo. Amina Hassan na taarifa kamili

(TAARIFA YA AMINA)

Mshirika hayo yakitoa mfano yamesema muda wa malori yanayoingiza bidhaa Rwanda  Afrika Mashariki, kusubiri kwenye vituo vya ushuru wa forodha umepungua kutoka siku 11 mwaka 2010 hadi saa 34 mwaka 2014,  kilichosaidia zaidi ni kupunguzwa kwa vituo vya ukaguzi na kusalia kimoja na hiyvo kuwasaidia wasafirishaji na watumiaji wa bidhaa Rwanda kuokoa dola milioni 6 kwa mwaka jana pekee.

WTO inasema hayo yamewezekana kutokana na mabadiliko ya taratibu za biashara na UNCTAD imekaribisha kuanza kutekelezwa kwa mkataba wa kimataifa wa kuwezesha biashara ikisema ni hatua kubwa katika kusonga mbele na kuifanya biashara kote duniani kuwa rahisi, ya gharama nafuu na ya haraka.

WTO inakadiria kwamba mkataba huo wa biashara utapunguza gharama za biashara kwa asilimia kati ya 9.6 na 23.1 kwa wanachama wake kote duniani nah ii itamaanisha ongezeko la dola kati ya bilioni 750 na trillion moja kwa usafirishaji nje bidhaa.