Skip to main content

Mustakhbali wa chakula mashakani kutokana na changamoto nyingi-FAO

Mustakhbali wa chakula mashakani kutokana na changamoto nyingi-FAO

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la chakula na kilimo FAO Jumatano imetoa onyo kwa jumuiya ya kimataifa kuhusu uwezo wa binadamu kujilisha katika siku za usoni.

Kwa mujibu wa takwimu za ripoti hiyo za mwenendo na changamoto katika mtazamo wa kila siku, zimebainika kwamba dunia itakabiliwa na kikwazo kikubwa katika kutimiza ajenda ya 2030 katika lengo la kutokomeza njaa.

Ripoti hiyo imeainisha mienendo 15 na changamoto 10 zinazohitajika kushughulikiwa ili kubadili hali hiyo. Lorenzo Bellu ni afisa wa masuala ya uchumi wa FAo anafafanua zaidi kuhusu mienendo hiyo

(SAUTI YA LORENZO BELLU)

“Kuna ukuaji wa uchumi ambao kwa bahati mbaya ni ukuaji unaohitaji rasilimali nyingi sana , nishaji, maji na kiasi Fulani ardhi, mwenendo wa pili ni idadi ya watu kwa hakika huenda tukafikia watu bilioni 10 katika muongo ujao nah ii inamaanisha kwamba chakula zaidi kinahitajika lakini pia rasilimali zaidi ya kukizalisha, na mwenendo mwingine ni kwamba haya yote hayatokeo katika dunia ya amani na usalama kinyume chake migogoro inaongezeka na hiki sio tunachotaka kukishuhudia”