Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sasa tusaidie Somalia ili ijikwamue- UM

Sasa tusaidie Somalia ili ijikwamue- UM

Nchini Somalia hii leo Rais Abdullahi Mohamed Farmaajo ameapishwa rasmi katika sherehe zilizoshuhudiwa na viongozi mbali mbali wa ndani ya nchi hiyo, Afrika, Ulaya na Umoja wa Mataifa, ikiwa ni baada ya kushinda uchaguzi tarehe nane mwezi huu. Taarifa zaidi na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora

Nats.. Gwaride! Nats.. Nyimbo! Nats…

Vilitawala hafla hii iliyofanyika kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, wageni wakiwa viongozi wastaafu wa serikali ya shirikisho, viongozi wa Afrika, Muungano wa Ulaya na Umoja wa Mataifa.

Salamu za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ziliwasilishwa na mwakilishi wake nchini humo, Michael Keating ambaye amesema uwepo wa pande zote hizo katika shughuli ya leo, ni kiashiria kuwa serikali hiyo mpya inaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa na hivyo akatoa wito kwa jamii hiyo kuendelea kusaidia nchi hiyo.

Amesema changamoto kama vile rushwa, ukame, njaa na udhaifu katika utawala vinahitaji ushirikiano baina ya wasomali wote hivyo akasema..

image
Michael Keating, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Somalia.(Picha:UNSOM)
(Sauti ya Keating)

“Wajumbe wa bunge jipya la shirikisho wana fursa ya kupitisha sheria zisizoegemea upande wowote na kwa wakati na kuwezesha serikali kukabili changamoto zinazokabili nchi.”

Na ndipo Rais Farmajoo akahutubia….

Nats..

Hotuba yake aliyotoa kwa lugha ya kisomali imejikita katika kusaka maridhiano, kutokomeza umaskini na masuala ya usalama kama kipaumbele cha serikali yake akisema kurejesha imani kwa serikali ni muhimu kwa wasomalia.