Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM, mashirika walaani kuzorota usalama CAR

UM, mashirika walaani kuzorota usalama CAR

Umoja wa Mataifa pamoja na jumuiya kadhaa ikiwamo Muungano wa Afrika AU, Jumuiya ya uchumi ya mataifa ya Afrika ya Kati ECCAS, wameelezea kusikitishwa kwao na kuzorota kwa usalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR. Taarifa kamili na Rosemary Musumba.

(Taarifa ya Rosemary)

Katika taarifa yao ya pamoja iliyohusisha pia Jumuiya ya Ulaya, na shirika la kimataifa la nchi zinazozungumza Kifaransa IOF, mashirika hayo yamesema yanatiwa shaka zaidi na hali katika wilaya za Quaka na Hautte-Kotto.

Mashirika hayo matano yamelaani ghasia za hivi karibuni zilizotekelezwa na kundi liitwalo FPRC na washirika wake pamoja na kikundi kingine kiitwacho UPC, ambazi zimesababaisha vifo vya raia kwa wingi na wengi kupoteza makazi, ilihali wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu tangu awali.

Yameeleza shukrani zao kwa hatua zinazochukuliwana ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini  humo MINUSCA, kwa mujibu wa mamlaka iliyopewa, za kulinda raia na kukomesha machafuko huku wakiutaka ujumbe huo kuendelea na wajibu huo.

Umoja wa Mataifa na wadau wake, wametaka kusitishwa kwa machafuko hima, pamoja na kuzingatia sheria za kimataifa za kibinadamu kwa kwa kuruhusu watoa misaada ya kibinadamu kuwafikia wahitaji.