Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Njaa yatishia pembe ya Afrika

Njaa yatishia pembe ya Afrika

Maeneo mengi ya ukanda wa pembe ya Afrika yanatarajiwa kupata mvua chini ya wastani na hivyo kutishia uhakika wa chakula na upatikanaji wa maji katika nchi ambazo zimeshuhudia ukame tayari, imefahamika leo.

Kwa mujibu wa ripoti ya jukwaa la hali ya hewa katika pembe ya Afrika, sababu ya ukame uliopo katika pembe hiyo unatokana na uhaba wa mvua msimu wa mwaka jana na kudorora kwa mvua msimu wa mwezi Machi hadi Mei mwaka huu, kimesema kituo cha utabiri wa hali ya hewa ICPAC ambacho kimeendesha jukwaa hilo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo hali inatarajiwa kuwa mbaya zaidi katika nchi ambazo tayari zimeshuhudia ukame ikwamo Somalia, Kenya Ethiopia na sehemu za Uganda, Sudan Kusini na Tanzania, ambako ukosefu wa maji unatarajiwa kwa kiwango kikubwa.