Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA inaisaidia Burkina Faso katika vita dhidi ya mbung’o

IAEA inaisaidia Burkina Faso katika vita dhidi ya mbung’o

Serikali ya Burkina Faso leo imezindua kitengo kikubwa kabisa Afrika ya Magharibi cha uzalishaji wa wadudu ili kutumia mbinu ya nyuklia kudhibiti mbung’o wadudu ambao wana madhara kwa binadamu na wanyama.

Kitengo hicho kimejengwa kwa msaada wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic, IAEA kwa ushirikiano na shirika la chakula na kilimo (FAO), katika hatua ya kusaidia kudhibiti moja ya magonjwa makubwa yanayoathiri vibaya ng’ombe , Nagana.

Kitengo hicho cha Bobo-Dioulasso ni kiwanda cha uzalishaji wadudu ambacho kitasaidia kanda hiyo kutumia mbinu ya SIT ambayo ni njia ya uzazi wa mpango kwa mbun’go hao kupunguza idadi yao. Njia hiyo inawafanya mbung’o dume kuwa tasa na hivyo kutozaliana.

IAEA imekuwa ikiisaidia Burkina Faso tangu miaka ya 1990 . Mbung’o huua zaidi ya mifugo milioni tatu kusini mwa jangwa la Sahara kila mwaka na kusababisha hasara ya dola bilioni 4.5 katika sekta ya kilimo.