Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zichukuliwe sasa kuokoa maisha Somalia-WFP/UNICEF

Hatua zichukuliwe sasa kuokoa maisha Somalia-WFP/UNICEF

Wakati ukame ukiighubika Somalia shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na lile la mpango wa chakula duniani WFP wameonya kwamba msaada pekee mkubwa ndio utalisaidia taifa hilo kuepuka kutumbukia katika zahma nyingine ya kibinadamu.

Taarifa ya pamoja ya mashirika hayo imesema ukame uliolikumba eneo la kaskazini mwa nchi hiyo mwaka jana sasa umesambaa Somalia nzima na kutishia mamilioni ya watu ambao tayari wameathirika na miongo kadhaa ya vita.

Watu milioni 6.2 ama hawana uhakika wa chakula au wanahitaji msaada na inatarajiwa watoto 944,000 watakabiliwa na utapia mlo mwaka huu.Laurent Bukera ni mkurugenzi wa WFP nchini Somalia

(LAURENT BUKERA)

Kuhusu hali ya watoto msemaji wa UNICEF Chrispother Boulierac amesema

(SAUTI YA BOULIERAC)