Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fedha zaidi zahitajika kuondokana na mabomu ya ardhini

Fedha zaidi zahitajika kuondokana na mabomu ya ardhini

Mradi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini umesema leo unahitaji dola milioni 511 kusaidia nchi zilizoibuka katika migogoro na zilizo katika migogoro kuondakana na idadi kubwa ya majeruhi ya mabomu hayo.

Taarifa kuhusu mradi huo imesema mahitaji hayo yameongezeka kwa kasi, sawa na asilimia 50% ikilinganishwa na mwaka jana, na ni picha halisi ya mikakati na mahitaji katika nchi 22 zilizoathirika zaidi na mabomu ya kutegwa ardhini, milipuko ya mizinga, makombora na silaha nyingine hususani katika bara la Afrika, Asia, Ulaya, Mashariki ya Kati na Amerika ya Kusini.

Fedha hizo zitatumika katika kuondoa mabomu hayo, kuelimisha kuhusu hatari zake, na kutoa msaada kwa waathirika na imesema kuna nia na maarifa lakini kilichosalia ni fedha.