Skip to main content

Radio yawezesha taarifa sahihi za hali ya anga kwa wakati sahihi

Radio yawezesha taarifa sahihi za hali ya anga kwa wakati sahihi

Radio ni zaidi ya burudani na ni muhimu kwa jamii hususan za wakulima na wafanyabiashara ambao tegemeo lao kupata taarifa ni chombo hiki adhimu. Ni kwa mantiki hiyo basi shirika la hali ya hewa duniani WMO limeangazia mradi wa kutoa taarifa za hali ya hewa kupitia radio na intaneti, RANET katika jamii nchini Kenya.

Katika makala hii Grace Kaneiya anatupeleka kaunti ya Murang'a ambako jamii wanategemea radio kupata taarifa mbali mbali ikiwemo hali ya anga ili kuweza kupanga shughuli mbali mbali za kujipatia kipato ikiwemo kilimo, ungana naye.