Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake Uganda wajitosa kwenye ufundi kujipatia kipato.

Wanawake Uganda wajitosa kwenye ufundi kujipatia kipato.

Wanawake nchini Uganda kama zilivyo sehemu nyingine, wanajitutumua kukabiliana na changamaoto za kazi katika ulimengu unaobadilika ili kujipatia kipato na pia kutimiza malengo ya usawa wa 50 kwa 50 kifikapo mwaka 2030.

Katika pitapita yake kutathimini kazi hizo kuelekea siku ya wanawake duniani Machi nane, John Kibego kutoka Uganda amekutana na mwanamke ambaye ndiye chanzo cha kipato cha familia kutokana na kazi za ufundi azifanyazo. Ungana naye.