Skip to main content

Sera za kutia moyo wakulima zahitajika ili kuimarisha upatikanaji chakula

Sera za kutia moyo wakulima zahitajika ili kuimarisha upatikanaji chakula

Benki ya dunia imesema kuimarisha kanuni za sekta ya kilimo katika nchi za vipato cha chini na kati ndio suluhu ya kuimarisha upatikanaji wa chakula ulimwenguni na kukwamua kipato cha wakulima.

Katika ripoti yake kuhusu kuwezesha biashara katika sekta ya kilimo, EBA ya mwaka 2017, benki hiyo imesema ingawa nchi nyingi zimeimarisha kilimo na hata kuweka fursa za kuuza nje mazao yao hatua zaidi zinahitajika.

Imetaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kupunguza gharama za biashara kwa wakulima na wafanyabiashara wanaouza ndani na nje ya nchi mazao yao na kuweka mazingira bora ya kupata mitaji kutoka taasisi za fedha.

Akizungumzia ripoti hiyo, Preeti Ahuja ambaye ni meneja wa masuala ya kilimo na chakula Benki ya dunia, amesema serikali zina dhima ya msingi ya kuweka sera zinazowezesha wakulima wadogo kushamiri na kuondoa gharama zinazovunja moyo washiriki wa sekta hiyo.