Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Radio yasalia mkombozi wa wengi

Radio yasalia mkombozi wa wengi

Radio! Chombo cha mawasiliano ambacho kila uchao kinazidi kupata umaarufu na wale ambao wamekizoea wanasema katu hawatoachana nacho kwani kinawapatia mambo makuu matatu; habari, elimu na burudani. Kuna baadhi ya watu wanaodai kuwa radio sasa si kitu tena, lakini si kwa wasikilizaji hawa ambao Anthony Joseph wa Radio washirika Uhuru FM kutoka Dar es salaam Tanzania amezungumza nao wakati akivinjari maeneo mbali mbali. Je radio inawasaidia nini wakati huu ambapo maudhui ya siku ya radio duniani tarehe 13 mwezi huu ni Radio ni wewe? Fuatana naye basi kwenye makala hii.