Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yakaribisha sheria ya kuhamishia uraia kwa watoto Madagascar

UNHCR yakaribisha sheria ya kuhamishia uraia kwa watoto Madagascar

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limekaribisha mabadiliko ya karibuni ya sheria ya utaifa nchini Madagascar, inayotoa haki sawa kwa wanawake na wanaume kuhamishia uraia wao kwa watoto.

Sheria hiyo mpya pia inasaidia wanandoa na watoto kusalia na uraia wao hata kama mmoja wa wanandoa au mzazi wanapoteza uraia huo.

UNHCR inasema mabadiliko hayo ni hatua muhimu katika kuchagiza kuzuia na kupunguza hali ya kutokuwa na utaifa.

Kimataifa nchi 89 zimetia saini mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 1954 unaohusiana na mambo ya kutokuwa na utaifa.