Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaonya mamilioni katika hatari ya baa la njaa Somalia

IOM yaonya mamilioni katika hatari ya baa la njaa Somalia

Zaidi ya watu milioni sita wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu nchini Somalia huku sehemu zingine zikitarajiwa kukumbwa na baa la njaa ndani ya miezi minne ijayo limesema leo shirika laUmoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.

Kwa mujibu wa shirika hilo hali ya mamilioni ya watu maeneo ya vijijini inazidi kuwa mbaya kutoka kwenye mgogoro na kuingia kwenye dharura kutokana na ukosefu wa chakula cha kutosha, maji, mifugo na huduma za afya.

Imeelezwa kuwa watoto takribani 363,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano wana unyafuzi na elfu 71 kati yao wako hatarini kupoteza maisha.