Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano lajadili vyombo vya habari, mitandao na kauli za chuki

Kongamano lajadili vyombo vya habari, mitandao na kauli za chuki

Huko Geneva, Uswisi hii leo kunafanyika kongamano la siku moja kuhusu kauli za chuki zinavyoenezwa kwenye vyombo vya habari dhidi ya wahamiaji na wakimbizi.

Akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa, Mwakilishi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ustaarabu, Nassir Abdulaziz Al-Nasser amesema kongamano linafanyika wakati muafaka wakati ambapo baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii huonyesha makundi hayo kuwa ni magaidi na  hata wanyonyaji wa fursa za kiuchumi kwa jamii kwenye nchi husika.

Amesema vyombo vya habari na mitandao ina nafasi kubwa kujenga mtazamo chanya wa jamii kwa makundi hayo, kwa hiyo..

(Sauti ya Nasser)

“Tutafanya kwa kadri ya uwezo wote kuelezea simulizi sahihi za wakimbizi ili kulinda maslahi ya jamii husika na pia haki za kila mtu. Nadhani mizania ni lazima iwepo ili kulinda uhuru wa kujieleza na vile vile haki za wahamiaji kama binadamu wenye haki.”