Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umuhimu wa maji kwa mustakhbali wa chakula duniani kumulikwa:FAO

Umuhimu wa maji kwa mustakhbali wa chakula duniani kumulikwa:FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO litakuwa kinara wa kutoa utalaamu na msaada wa kiufundi kwenye kongamano la kimataifa la chakula na kilimo litakaloanza kesho tarehe 19 Januari hadi tarehe 21 Januari mjini Berlin, Ujerumani.

Kwa mujibu wa FAO kila Januari kwa takriban muongo mmoja sasa mji wa Berlin umekuwa mahala pa kukusanyika wadau wakubwa wa kilimo duniani. Mwaka huu kongamano hilo la chakula na kilimo lililoandaliwa na wizara ya chakula na kilimo ya Ujerumani , kauli mbiu yake ni "kilimo na maji , ni kitovu cha kuilisha dunia'.

FAO itawakilishwa na Mkurugenzi wake Mkuu José Graziano da Silva, ambaye pia atashiriki katika mkutano wa mawaziri wa kilimo na kukutana na waandishi wa habari siku ya Jumamosi na kuhudhuria kikao cha mawaziri wa kilimo kutoka nchi zilizoendelea za G20 siku ya Jumapili.