Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatari mpya ya ukame yaighubika Ethiopia:FAO

Hatari mpya ya ukame yaighubika Ethiopia:FAO

Ukame mpya uliolikumba bonde la Kusini mwa Ethiopia huenda ukaathiri kurejea kwa uhakika wa chakula katika taifa hilo la Afrika Mashariki endapo hatua madhubuti hazitochukuliwa, baada ya kuwa na msimu mbaya zaidi wa kilimo kwa miongo kadhaa limeonya leo shirika la chakula na kilimo FAO.

Wakati juhudi za serikali zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza madhila ya kibinadamu na njaa wakati wa ukame mkali kuwahi kulikumba taifa hili kwa karibu nusu karne, athari za El Niño na uhaba wa mvua vinatoa tisho jipya hususani kwa jamii za wafugaji ambao wanashuhudia uhaba wa malisho na maji katika majimbo ya Kusini mwa nchi hiyo.

FAO inasema jumla ya dola milioni 42 zinahitajika kwa ajili ya sekta ya kilimo ili kuwasaidia wakulima na wafugaji katika kaya milioni 1.9 hasa katika majimbo yaliyoathirika zaidi ya wafugaji kwa mwaka huu.