Skip to main content

“Kiasi” kuna ahueni katika ukuaji wa uchumi wa dunia

“Kiasi” kuna ahueni katika ukuaji wa uchumi wa dunia

Mwaka 2017 utashuhudia kiasi ahueni katika ukuaji wa uchumi duniani kwa mujibu wa idara ya uchumi na masuala ya jamii ya Umoja wa Mataifa DESA.

Matumaini hayo yamo kwenye ripoti inayoelezea hali ya uchumi na matarajio duniani mkwa mwaka 2017. Pia imetoa suluhu ya kipindi kirefu cha mdororo wa uchumi uliosababishwa na uwekezaji duni na ukuaji hafifu wa biashara ya kimataifa.

Lenni Montiel ni msaidizi wa Katibu Mkuu kwa masuala ya maendeleo ya uchumi DESA. Anaainisha masuala muhimu yaliyobainiwa na ripoti hiyo

(LENNI CUT)

“Uchumi wa dunia umeendelea kughubikwa na ukuaji mdogo. Mwak a 2016 ukuaji wa pato la taida duniani ulishuka hadi asilimia 2.2 na huo ukikuwa ni ukuaji mdogo sana tangu mdororo wa uchumi wa 2009.Pia uzalishaji mdogo pamoja na kiwango kikubwa cha madeni vimekuwa vikiathiri mwenendo mzima wa ukuaji”

Sasa nchi wanachama wazingatie nini ili kuinua uchumi huo?

“Tunahitaji kusistiza juhudi za sera imara ili kuchagiza uwekezaji na uzalishaji , kwa ujumla sera mizania zinahitajika ikimaanisha tunahitaji kuendelea na ufuatiliaji wa sera za msaada , tunahitaji sera zinazofanya kazi , na yote hayo ynahitaji kwenda sanjari na mabadiliko katika mifumo ya uchumi ya nchi nyingi”