Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres kuzuru Uswisi Januari 17-21

Guterres kuzuru Uswisi Januari 17-21

Katibu Mkuu wa moja wa Mataifa António Guterres atakuwa ziarani Uswisi kuanzia Kesho Jumanne Januari 17 hadi Januari 20 mwaka huu.

Katika ziara hiyo Guterres atakuwa na mkutano usio rasmi na waandishi wa habari Jumatano, atakutana na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Geneva, na pia kuwa na mkutano na wafanyakazi kabla ya kukutana na maafisa wa serikali ya Uswis.

Kabla ya kuwa na mkutano wa ngazi ya juu, Bwana Guterres atafanya mazungumzo na Rais wa Uchina Xi Jinping na Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Peter Thomson .

Kisha Alhamisi Januari 19 Katibu mkuu ataelekea Davos kuhudhuria kongamano la kimataifa la uchumi, ambako atashiriki kikao maalumu atakachobainisha mtazamo wake kwa ajili ya Umoja wa Mataifa kuhusu ushirikiano kwa ajili ya amani na kukabiliana na mizizi ya migogoro ya kimataifa.

Pia anatarajiwa kukutana na viongozi mbalimbali wa dunia kabla ya kurejea New York Januari 20.