Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iran yahamisha vifaa vya kuzalisha nyuklia-IAEA

Iran yahamisha vifaa vya kuzalisha nyuklia-IAEA

Shirika la nishati ya atomiki duniani, IAEA limesema Iran imeondoa vifaa na miundombinu ya ziada inayohusiana na mchakato wa kuzalisha nishati ya nyuklia kwenye mtambo wa Fordow.

Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Dkt. Yukia Amano amesema hayo katika taarifa yake iliyotolewa hii leo akisema walithibitisha utekelezaji huo tarehe 15 mwezi huu.

Amesema hatua hiyo ni kwa mujibu wa ahadi iliyotolewa na Iran kupitia mpango thabiti wa pamoja wa utekelezaji JCPOA.

Mpango huo unataka ndani ya mwaka mmoja, Iran iwe imekamilisha uondoaji wa vifaa hivyo vya ziada kutoka mtambo huo na kuhifadhi kwenye mtambo wa Natanz ulio chini ya uangalizi wa IAEA.