Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rwanda, Kenya, Chad ni mfano wa udhibiti matumizi ya tumbaku

Rwanda, Kenya, Chad ni mfano wa udhibiti matumizi ya tumbaku

Shirika la afya duniani, WHO limesema sera bora za kudhibiti matumizi ya tumbaku zina manufaa makubwa kiuchumi na kijamii.

WHO imetaja sera hizo ni pamoja na kuongeza ushuru kwenye bidhaa za tumbaku na udhibiti wa matumizi na hivyo mapato kutumika katika shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii.

Akihojiwa na Idhaa hii Dkt. Ahmed Ouma, mshauri wa masuala ya tumbaku ofisi ya WHO kanda ya Afrika amefafanua mafanikio hayo..

(Sauti ya Dkt. Ouma)

Amesema Rwanda, Kenya, Chad, Mauritius zimejumuisha sera za udhibiti kwenye bajeti na wakulima wa tumbaku wanahamasishwa kilimo mbadala..

(Sauti ya Dkt. Ouma)