Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yawawekea wakimbizi wa Syria fedha kwenye akaunti kwa ajili ya chakula .

WFP yawawekea wakimbizi wa Syria fedha kwenye akaunti kwa ajili ya chakula .

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP, leo limeingiza dola milioni 9.8 kwenye akaunti za kwa wakimbizi wa Syria nchini Lebanon. Fedha hizi ni mchango kutoka Canada na itawafaidisha zaidi ya watu 310,000 ambao wanategemea msaada wa kibinadamu.

Naibu wa Mwakilishi wa WFP nchini Lebanon Paul Skoczylas ameishukuru serikali ya Canada kwa mchango huo utakaowasaidia mamia ya maelfu ya wakimbizi kwenye mazingira magumu wakati huu wa msimu wa baridi kali.

Karibu asilimia 93 ya wakimbizi wa Syria wanaoishi nchini Lebanon wanakabiliwa na ukosefu wa chakula, ili kujitosheleza WFP inawapatia msaada pesa kwenye kadi za elektroniki zitakazowawezesha kununua chakula wanachohitaji katika maduka 490 kote nchini.

Kadi hiyo moja inatumiwa na mashirika ya mengine ya Umoja wa Mataifa ambayo n ilile la kuhudumia watoto UNICEF,na la kuhudumia wakimbizi UNHCR .