Guterres azungumza na Trump

Guterres azungumza na Trump

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amekuwa na mazungumzo kwa njia ya simu na Rais mteule wa Marekani Donald Trump kuhusu masuala kadhaa ikiwemo uhusiano wa nchi hiyo na Umoja wa Mataifa.

Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema hayo leo akizungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani, kufuatia swali lililowasilishwa kwenye ofisi yao.

(Sauti ya Farhan)

“Naweza kuthibitisha Katibu Mkuu amekuwa na mazungumzo na Rais mteule Trump jumatano asubuhi. Ilikuwa ni simu ya kujitambulisha amapo walikuwa na mazungumzo chanya kuhusu uhusiano kati ya Marekani na Umoja wa Mataifa. Katibu Mkuu amesema anasubiri kwa hamu kushirikiana na Rais huyo baada ya kuapishwa kwake.”