Umoja wa Mataifa walaani mashambulizi Iraq

31 Disemba 2016

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  ni Iraq chini Ján Kubiš, amelaani mashambulizi mawili ya mabomu jijini Baghdad hii  yaliyosabisha vifo na majeruhi.

Katika tarifa yake kiongozi huyo amesema katika siku ya mwisho wa mwaka 2016, wakati watu wa Iraq wakijiandaa kuupokea mwaka mpya kwa matumaini ya amani, magaidi walishambulia tena raia wasio na hatia.

Kubiš amesema kitendo hicho ni cha kupuuzwa na wahusika wafikishwe kwenye mkono wa sheria haraka iwezekanavyo.

Ametuma salamu za rambirambi  kwa familia za wale walipoteza wapendwa wao na kuwatakia uponyaji wa haraka majeruhi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter