UNESCO yalaani mauaji ya mchapishaji na mwandishi wa habari

UNESCO yalaani mauaji ya mchapishaji na mwandishi wa habari

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, Irina Bokova, ametaka  uchunguzi wa kina kufuatia mauaji ya mchapishaji na mwandishi wa habari Larry Que nchini Ufilipino. Huku akilaani pia mauaji hayo, Bokova ametaka wahusika wafikishwe mbele ya sheria.

Taarifa hiyo ya UNESCO inasema kuwa mwandishi huyo alipigwa risasi mnamo Desemba 19 katika mji wa Virac katika jimbo la kati la Catanduanes na akafaa Desemba 20 kutokana na majeraha aliyoyapata.

Bi Bokova ameongeza kuwa waandishi wa habari lazima kuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa hali ya usalama ili kuhakikisha uhuru wa habari  na kwa jamii kwa ujumla usalama wao kulindwa.

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO hutoa matamshi kuhusu mauaji ya wafanyakazi wa vyombo vya habari sambamba na Azimio 29 iliyopitishwa na nchi wanachama wa UNESCO.