Watu 100 waripotiwa kuzama Mediteranea- UNHCR

23 Disemba 2016

Takribani watu 100 wameripotiwa kuzama kwenye bahari ya Mediteranea siku ya Alhamisi katika matukio mawili tofauti na hivyo kufanya idadi ya watu waliozama baharini humo kwa mwaka huu kuvuka Elfu Tano. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Assumpta)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema idadi hiyo ni kubwa kuwahi kushuhudiwa na kwamba boti mbili za kujaza upepo zikiwa na abiria wapatao 260 zilipasuka na abiria wakatumbukia baharini.

William Spindler, msemaji wa UNHCR Geneva, Uswisi amesema maiti wanane wameokotwa huku watu 143 wakiokolewa na walinzi wa pwani.

(Sauti ya Spindler)

“Hali hii inadokeza udharura wa nchi kuongeza fursa za kuruhusu wakimbizi kuingia kama vile kuwapatia makazi, ufadhili binafsi, kuungana kwa familia na mifumo ya usaidizi wa mafunzo kwa wanafunzi ili waepuke safari za hatari na kutumiwa na wasafirishaji haramu wa binadamu.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter